December 1, 2018


Mshambuliaji  wa kimataifa wa timu ya Simba raia wa Rwanda, Meddie Kagere anajua kwamba wapinzani wao Yanga wanaongoza ligi kwa sasa wakiwaacha nyuma kwa jumla ya pointi 8, ameibuka na kuwatuliza mashabiki wa Msimbazi.


 

Simba wamecheza michezo 12 na kujikusanyia pointi 27 baada ya kushinda mechi 8 sare 3 na kupoteza mchezo 1 wakiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu.

 Kagere amesema kuwa hana wasiwasi na wapinzani wao Yanga kuongoza ligi kwa sababu anajua walichokifanya mpaka wakawa hapo na wao wanatakiwa kufanya nini.

"Sina wasiwasi na wanaoongoza Ligi kwa sasa kwa sababu najua kile ambacho wamekifanya na sisi tunatakiwa kufanya nini ili tuweze kufika hapo walipo hakuna cha kuhofia.


"Wao wameshinda michezo yao na ndio maana wapo hapo hivyo ili nasi tuweze kufika hapo walipofika kazi yetu ni moja tu kushinda michezo yetu hicho tu hakuna kingine," alisema Kagere.


Kagere ana jumla ya mabao 7 kwenye ligi kuu msimu huu pia ni mchezaji wa kwanza kuchukua tuzo ya mchezaji bora ligi kuu iliyotolewa na kamati ya tuzo mwezi Agosti.



BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS

Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo akikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.

Asante

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORT

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic