December 19, 2018



Kikosi cha Simba kitakachoanza leo Desemba 19 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC uwanja wa Taifa saa 12:00 jioni kimekuwa na sura mpya kama ambavyo Ofisa habari Haji Manara alisema Jana.

Mlinda mlango namba mbili wa Simba, Deogratius Munish 'Dida' amefanikiwa kupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha Simba pamoja na Zana Coulibarly ambaye ni beki mpya raia wa Burkina Faso.

Beki Kiraka wa Simba Erasto Nyoni kabla ya mchezo alisema kuwa wamejipanga vizuri kupata matokeo baada ya kupata mbinu kali kutoka kwa kocha mkuu Patrick Aussems.

Simba wameheza michezo 12 na leo wanafikia mchezo wa 13 wakiwa wameachwa kwa jumla ya pointi 17 na vinara wa Ligi Yanga wenye pointi 44 kwa sasa wakiwa wamecheza michezo 16.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic