December 19, 2018


Mahakama imeutaka upande wa serikali ambao unasimamiwa na  mawakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  kuwa  makini na kesi ambayo inawakabili waliowahi kuwa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamali Malinzi na Celestine Mwesigwa.

Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, iliahirishwa kufuatia Wakili wa Serikali, Leonard Swai kuomba kesi hiyo ihairishwe kufuatia shahidi waliyemuandaa kuwa na  udhuru wa kifamilia, hivyo ameomba muda ili kuweza kuandaa shahidi mwingine atakayetoa ushahidi katika kesi hiyo.

Kufuatia, maombi hayo ya upande wa mashitaka ambao ni Takukuru kutaka kesi kuahirishwa, jopo la mawakili wa upande wa washitakiwa chini ya kiongozi wake, Richard Rweyongeza imeitaka Mahakama ichukue hatua kwa upande wa mashitaka kufuatia kushindwa kutekeleza amri ya mahakama.

Aidha walieleza kuwa, kama hawana ‘Interest’ na kesi hiyo ni bora wawaachie washitakiwa  kwa kuwa wamekaa sana rumande ikiwa ni miaka miwili sasa ikiwa ni pamoja na kushindwa kutekeleza amri ya mahakama iliyotolewa kwa kuandaa mashahidi watatu badala ya mmoja ambaye ameshindwa kufika.

Pia wameiomba mahakama kuweza kuliangalia suala hilo kwa kuhakikisha kesi inasikilizwa mfululizo ndani ya siku tatu huku ikiitaka kuchukua hatua kwa upande wa mashitaka kutokana na kutekeleza amri hiyo ya mahakama.

Kwa kuzingatia  maelezo ya pande zote mbili, Mahakama chini ya Hakimu Mashauri, aliamua kuahirisha kesi hiyo na kutoa maamuzi ya kusikilizwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 16, 17 na 21 Januari, Mwakani, huku akiutaka upande wa mashitaka kuwa siriasi na kesi hiyo ili kuweza kukamilisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic