December 3, 2018


Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makmabo ambaye kasi yake ya kufunga imewashtua wengi kutokana na kuweza kufunga mfululizo katika mechi tatu alizocheza hivi karibuni amefichua siri ya mafanikio.

Makambo amefikisha mabao 7 sawa na washambuliaji wa Simba Meddie Kagere na Emanuel Okwi huku kinara akiwa ni mzawa Eliud Ambokile mwenye mabao 9 kwa sasa.


Makambo amesema anatambua mashabiki wanahitaji matokeo mazuri ili wawe na furaha na ndio maana wakati anashindwa kuisaidia timu kupata matokeo walikuwa wanamsema vibaya ila hakukata tamaa.


"Mashabiki walikuwa wananisema ila haikunifanya niweze kutoka kwenye mchezo, nilijitahidi kuendelea kufanya mazoezi na kujituma zaidi, ushirikiano ambao upo ndani ya timu unatufanya tuzidi kupata matokeo," alisema.


Mechi tatu za karibuni ambazo Makambo alifunga ni dhidi ya  Mwadui FC ya Shinyanga, Kagera Sugar na JKT Tanzania ambapo mabao yake yote alifunga kipindi cha kwanza leo atakuwa kibaruani kuwavaa Prisons ya Mbeya.


Kutoka Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic