December 3, 2018



Baada ya mchezo wa jana kati ya Lipuli na Biashara United kuahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha mchezo ulipoanza, kocha wa Lipuli Seleman Matola amesema kuwa mipango mingi imevurungika hivyo leo anaanza upya.


Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Samora, Iringa ulivunjika baada ya kuchezwa kwa muda wa dakika 26 na timu hizo kutoka sare ya kutofungana hivyo leo saa 8 mchana watamalizia dakika 64 zilizobaki.


"Kwa kiasi fulani imetibua mipango yangu hasa kutokana na ukweli tulianza kuchanganya kwa timu yetu kuweza kupata nafasi za kushambulia pamoja na mwenendo mzuri hivyo inanipasa leo kuanza upya.


"Kuna faida na hasara kwa mchezo kusimama kwa muda kama ilivyotokea kwetu kwa kuwa najua wameshasoma mbinu zetu nasi tumeweza kujua namna ambavyo walivyo hivyo muda mwingi watakuwa wametafuta mbinu za kutuzuia," alisema.

1 COMMENTS:

  1. Kwhy bado mnatumia picha za Mgambo fc..mnakera sana yani nyie mmejaa uvivu tuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic