December 6, 2018


Na George Mganga

Aliyewahi kuwa mchezaji wa Yanga, Ally Mayay, amewataka Simba kujipanga vilivyo kuelekea mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia.

Simba itakutana na Nkana ambayo pia imefuzu jana kwa kuitoa UD Songo ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 3-1.

Kwa mujibu wa Radio EFM kupitia E Sports, Mayay amesema Simba wanapaswa kuwa na tahadhari ili kuhakikisha wanafanya vizuri dhidi ya Nkana akieleza wapo vizuri kuliko Mbabane Swallows.

Mayay amewashauri Simba kujipanga vema kwani ubora wa Nkana ni wa tofauti zaidi na Mbabane ambao waliwafunga kwa jumla ya mabao 8-1.

"Ni vema Simba wakaenda kucheza mechi hiyo kwa tahadhari kubwa kwani Nkana ni timu nzuri kuliko hata Mbabane, wana uzoefu na mashindano na wamekuwa wakifanya vema katika mashindano ya kimataifa" alisema.

Simba na Nkana zitakutana kati ya Disemba 15 au 16 na mechi ya marudiano itafanyika kati ya Disemba 27 na 28 mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic