December 6, 2018


Baada ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, kucheza mechi tatu nje ya Dar, timu hiyo imefanikiwa kuweka rekodi ya dakika 270 ambazo ni sawa na mechi hizo tatu, huku akimpoteza Mbelgiji wa Simba, Patrick Aussems.

Yanga kwa sasa imecheza jumla ya mechi 14, kati ya hizo, tatu pekee ndizo imecheza nje ya Dar ambapo ni Shinyanga, Kagera na Mbeya. Katika mechi hizo, imekusanya jumla ya pointi tisa.

Kocha Mwinyi Zahera raia wa DR Congo akiwa katika mazoezi na wachezaji wake.

Yanga ilianza kwa kuifunga Mwadui mabao 2-1 katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, kisha ikaibuka na ushindi kama huo mbele ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Jumatatu ya wiki hii, ikaibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Prisons, Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Hii inakuwa ni rekodi mpya kwa timu hiyo ndani ya msimu huu ikiwa chini ya kocha Mwinyi Zahera raia wa DR Congo licha ya awali kuelezwa timu hiyo isingeweza kufanya vizuri kwenye mechi za mikoani kutokana na kupita kwenye hali ngumu ya kiuchumi.

Kwa upande wa Simba ambayo ipo chini ya kocha Patrick Aussems, imecheza michezo minne mkoani ambapo walitoka sare na Ndanda ya Mtwara 0-0, ikifungwa na Mbao 1-0, ikashinda 3-1 dhidi ya Mwadui na ikashinda 2-0 dhidi ya JKT Tanzania.

Hivyo katika mechi hizo nne, Simba wameshinda mbili wametoka sare moja na kufungwa moja tofauti na Zahera ambaye kwenye tatu ameshinda zote.

5 COMMENTS:

  1. Mimi nilidhani Simba alifungwa mechi zote alizocheza mikoani kumbe alipoteza mchezo mmoja tu? Halafu mnatunga vichwa vya habari vya hovyo tena ligi ingali bado mbichi kabisa sijui kama Yanga ndio ingekuwa imempiga mtu kimataifa weekend na ushehe ingekuwaje?

    ReplyDelete
  2. Acha waendelee kuwaza kucheza na mwadui na mbao, cc tunawazia timu za kimataifa. Uandishi wa kishabiki pia ni kawaida ya blog hii. Wangeshinda wao kimataifa nadhani hii blog isingelala, lakini jaribu kuangalia taarifa ambazo jamaa wamezitoa kuhusu ushindi wa simba huko eswatini juzi, jana hadi saa 12 jioni ni taarifa mbili tu zinazohusu ushindi wa simba, ingekuwa Yanga Blog ingekesha inatengeneza stori tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona povu linawatoka sana nyie mabwege......mnataka mpigiwe matarumbeta barabarani ndo ijulikane kuwa mmeshinda......halafu unasema eti "waache waendelee kuwaza kucheza na mwadui na mbao,sisi tunawazia timu za kimataifa".........umesahau kuwa huwezi kucheza kimataifa bila kumfunga huyo mbao na mwadui unaowadharau?.......umesahau kuwa huyohuyo mbao unaemdharau ndo alikuaibisha hapa kwenye ligi,tukisema mbao ni timu bora kuliko hiyo ulokutana nayo kimataifa tutakuwa tumekosea?.......pia usijisahaulishe kuwa wakat yanga anashiriki mashindano ya kimataifa kwa miaka mitatu mfululizo,wewe ulikuwa ukirukaruka tu kwenye hiihii ligi unayoidharau leo bila kupata ubingwa wa kukupeleka kimataifa.

      Delete
    2. @Erick Ndunguru, Ya kale hayanuki babuuuuuuuuu........... hiyo ya kimataifa kwenu VYURA FC itabaki ni story tu. Mtaendelea kubaki hapa hapa tu. Hiyo Simba unayoizungumzia miaka hiyo, ni simba iliyokuwa na uongozi wa aina kama ya VYURA FC, Simba ya sasa ni ya kimataifa kuanzia uongozi namna ya uendeshaji hadi soka linalotandazwa uwanjani, inafikia wenye simba yetu tunaona dakika tisini ni chache, labda FIFA waongeze dakika za kawaida za mchezo walau ziwe hata 120 ili burudani iendelee kububujika katika nafsi zetu. Nyinyi VYURA FC Mwanzo wa ligi hadi mwisho ikitokea sana mmejitahidi kukaza matako mtaishia nafasi ya tatu, lakini nafasi mnayostahili kwa hapa bongo ni nafasi ya tano na nne tu. Na wewe huyu jamaa mwenye Blog akikuajiri uwe unamkusanyia taarifa za michezo, nadhani mtaendana sana.

      Delete
  3. Enter your comment...simba sc niyakimataifa saiz saiz cc tunawaza kucheza ns Nkana cyo mwadui tna hii ni simba ya Mo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic