KOCHA WA AISHI MANULA ATOA UJUMBE KUELEKEA MECHI NA NKANA
Na George Mganga
Kocha wa makipa Simba, Mwarami Mohammed, amesema maandalizi yao kuelekea mechi na Nkana kesho yamekamilika.
Mohammed ameeleza wameshawaandaa wachezaji wao kwa ujumla vizuri na wapo tayari kupigana kufa na kupona ili kuweza kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Ameweka wazi maandalizi yao yamezingatia kwa lengo kubwa la kuweka historiampya kwenye mashindano haya makubwa kwa ngazi ya vilabu Afrika.
“Tumewaanda wachezaji vizuri tayari kwa mchezo ili tupate ushindi na tuandike historia mpya, ni mchezo muhimu sana kwa klabu.
Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi ikiwezakana tuujaze kabisa uwanja”, amesema.
Kocha ajitathmini...Manura kiwango kinaporomoka
ReplyDeleteMfundishe Manula kujitambua anapo kuwa golini amekuwa na udhaifu wa mashuti ya mbali anafungwa kila mara,aje kujipanga pia inaonekana ni nzito kuyafuata yani hajirushi mzimamzima.
ReplyDeleteni kweli kabisa
Delete