December 26, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametengua kauli zilizoelezwa kuwa amemsamehe kipa Beno Kakolanya kurejea kikosini.

Zahera ambaye hivi sasa ameshaanza safari ya kurejea nchini, amedai kilichoelezwa kuwa amemsamehe mchezaji huyo ni uzushi na hakuna ukweli wowote ule.

Mkongomani huyo ameendelea kuonesha msimamo wake akifunguka hataweza kuubadili kamwe kutokana na kutopendezwa na tabia za Kakolanya ikiwemo kugomea mazoezi.

Kakolanya alikataliwa na Zahera baada ya kugomea kusaifri na timu akidai malipo ya fedha zake za usajili na mshahara jampo ambalo lilimuudhi Mkongomani huyo.

Zahera alisema yeye kama Kocha amekuwa akijitoa kwa Yanga ambayo inapitia wakati mgumu hivi sasa na hakuna sababu ya mchezaji kugoma kisa mshahara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic