December 28, 2018


UONGOZI wa KMC umesema unatambua ugumu wa mchezo wao wa leo dhidi ya Mbao FC utakaochezwa uwanja wa Uhuru, hilo liwapa hasira kuelekeza nguvu kupata pointi tatu muhimu.

Ofisa habari wa KMC, Anwari Binde amesema ugumu  huo unatokana na ukweli kwamba kocha Mkuu wa KMC, Ettiene Ndayiragije alikuwa kocha wa Mbao awali hivyo mbinu zake zipo wazi kwa wapinzani wao.

"Ushindani utakuwa mkubwa ukizingatia kwamba mbinu zetu zipo mikononi mwa Mbao, tumejipanga kupata matokeo na muda utazungumza uwanjani kocha ametoa mafunzo makini yatakayosaidia wachezaji kutafuta matokeo," alisema.

KMC wamekuwa na matokeo mazuri hivi karibuni baada ya kupanda daraja kwa kuwa ipo ndani ya 10 bora kwenye msimamo ikiwa inashika nafasi ya 9 ikiwaacha mbali Tanzania Prisons ambao msimu uliopita walimaliza wakiwa nafasi ya nne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic