December 28, 2018


MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand United aliyepata umaarufu ghafla baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 3 msimu huu 'hat trick' Alex Kitenge ameondoka kwenye kikosi hicho na kudai kwamba anapata taabu ndani ya kikosi hicho kutokana na kutolipwa.

Kitenge hakuwa na bahati tena ya kufunga licha ya kucheza kwenye michezo mingine ya Ligi akiwa na timu yake kwa kile alichoeleza kuwa ni kukamiwa na mabeki wa timu pinzani.

"Kwa sasa nipo Burundi, sina mpango wa kurejea bongo kwa kuwa sijalipwa kwa muda mrefu stahiki zangu nikiwa Stand United, bado hali ni ngumu hivyo nitareea mipango ikikaa sawa ndani ya kikosi," alisema.

Stand United wamecheza michezo 17 kwenye Ligi kuu na kufanikiwa kukusanya pointi 18 ambazo zinawafanya washike nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic