December 19, 2018


Wanachama nane wa Yanga wanachunguzwa na Serikali kwa  kudaiwa kuwashinikiza wenzao kwa ajili ya kugomea uchaguzi wa timu hiyo usifanyike kutokana na kuendelea kumtambua Yusuf Manji kama mwenyekiti wa timu hiyo.

 Mkurugenzi wa Michezo Tanzania, Yusuph Singo amesema wameamua kuwachunguza wanachama hao baada ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuyapata jana usiku kuwa wanawashinikiza wanachama wenzao kugomea uchaguzi wa klabu hiyo ambao umepangwa kufanyika Januari 13, mwakani.

“Jana Waziri Mwakyembe amepokea majina ya wanachama nane ambao wanaleta vurugu ili uchaguzi wa Yanga usifanyike ambapo wanachama hao wanapinga kujiuzulu kwa Yusuf Manji.

“Baada ya kuyapata majina hayo, yamepelekwa kwa vyombo vya usalama na kama ikibainika kwamba wamefanya hivyo basi hatua kali sana zitatolewa ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa wakipinga juu ya uchaguzi huu licha ya kwamba kumefanyika njia ya kidemokrasia na pande zote kukubali kwamba uchaguzi ufanyike.

“Serikali tunaiagiza TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) na BMT (Baraza la Michezo la Taifa) kusimamia uchaguzi huu na unafanyika kama ulivyopangwa na tunawaambia wanachama wa Yanga wawe watulivu na wajitokeze kwa wingi wakachague viongozi siku ya uchaguzi kwa sababu Yanga haiwezi kuwa imara bila ya viongozi.

"Wanachama hao ni pamoja na Mustapha Mohammed, Edwin Kaisi, Said Bakari, Shaban Omari, Kitwana Kondo Kipwata, Boazi Ikupilika, Bakili Makere na David Sanare na watachuuliwa hatua kali ukweli ukibainika," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic