December 7, 2018






Kocha Mkuu wa Mbao FC Amri Said amewapa mbinu wachezaji wake wote ili kuhakikisha wanafanikiwa kuvunja rekodi ya timu ya Azam ambayo mpaka sasa haijapoteza hata mchezo mmoja katika michezo 14 waliyocheza.

Evarist Mujahukwi ambaye ni Super Sub wa muda wa kikosi cha Mbao FC amesema kuwa wamejipanga kuweza kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo dhidi ya Azam FC.

"Tumejiandaa vizuri kiakili na kisaikolojia pia, kocha ametupa mbinu bora zitakazotusaidia kuweza kupindua meza kibabe leo, hivyo mashabiki watupe sapoti tutakapokuwa uwanjani kutafuta matokeo," alisema.

Mbao FC wanashika nafasi ya 8 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 14 wameshinda 5 sare 5 na wamepoteza michezo 4 na kujikusanyia pointi 20. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic