December 25, 2018


Mwekezaji Mkuu wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo' amegawa mamilioni kwa kikosi cha Simba baada ya kuwatoa Nkana Red Devils katika Ligi ya Mabingwa Afrika, imeelezwa.

Taarifa imesema Mo ametoa kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 84 ambazo ni kama motisha kwa wachezaji hao waliopigana kufa na kupona kupindua matokeo.

Katika mchezo wa kwanza ambao Simba walicheza ugenini waliweza kufungwa mabao 2-1 lakini walifanikisha kupindua kwa kuwachapa Nkana 3-1 jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo inaelezwa pia bosi Mo ameahidi mpunga mwingine tena kwa kikosi hicho kuelekea hatua inayofuata ya ligi hiyo kubwa kwa Afrika.

Hivi sasa Simba inasubiria kujua itapangwa na timu ipi katika hatua ya makundi siku ya Ijumaa ambapo droo hiyo itafanyika Ijumaa ya wiki hii huko Cairo, Misri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic