December 25, 2018


Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba upo kwenye mikakati ya kugawa vikosi vyake kwa ajili ya kupata nafasi ya kuvitumia katika mashindano mbalimbali inayoendelea hivi sasa.

Maamuzi hayo yanakuja kutokana na ujio wa mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kuanza Disemba 31 huko visiwani Zanzibar huku Simba ikiwa ni moja ya timu zitakazoshiriki.

Taarifa zinasema Simba watavigawa vikosi huku kimoja kikienda Zanzibar na kingine kikisalia Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika inayopewa kipaumbele kikubwa.

Simba ambayo imefuzu kuingia hatua ya makundi, inasubiria droo ya kupangwa kwa makundi hayo ambayo itafanyika Ijumaa ya wiki hii jijini Cairo, Misri.

Aidha, kikosi cha Simba kesho kitashuka dimbani kucheza na Mashujaa United kutoka Kigoma katika mchezo wa kwanza wa Kombe la FA msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic