December 25, 2018


Mabosi wa Simba wapo kwenye mipango ya kumalizana na aliyekuwa Kocha wa Mbao FC, Amri Said 'Stam' kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Masoud Djuma.

Stam ambaye aliwahi pia kuifundisha Lipuli kabla ya kutimkia Mbao ya Mwanza, ameingia kwenye rada za Simba ikiaminika anaweza akaitendea vema kikosi hicho.

Taarifa zinasema Stam atakuwa na kikosi cha Simba kitakachokwenda Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Mapinduzi Cup pamoja na SportPesa Super hapo baadaye ambayo itafanyika hapa Tanzania.

Mpaka sasa Simba hawajataka kuliweka suala hili wazi kwa kina ila habari za uhakika zinasema inaweza ikaingia naye mkataba muda wowote kuanzia sasa.

Stam akiingia Simba atachukua rasmi nafasi ya Djuma ambaye aliondoshwa baada ya kuwa sehemu ya mtafaruku baina yake na Kocha Mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic