December 23, 2018


Kuelekea mechi kubwa ya leo katika Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhdi ya Nkana Red Devils ya Zambia, unaambiwa jana baadhi ya mashabiki wa Yanga walijitokeza kwenye Uwanja wa Taifa wakiwa na dhumuni ambalo halikujulikana ni lipi.

Mashabiki walikuwa wakidai wanataka kuingia Uwanjani kwa lengo la kufanya kikao mpaka ikapelekea wenzao wa Simba kuwadhibiti vikali ili wasiwezi kwenda ndani.

Ilielezwa kuwa walikuwa na lengo la kuingia uwanjani kisha kufanya mambo yanayohusiana na imani za kishirikina mpaka ilipelekea shabiki mmoja wa Yanga kupigwa na kutokwa na damu mdomoni.

Shabiki mmoja wa Simba 'jina tunalo' alisema mashabiki hao wa Yanga walikuwa hawana nia njema na uwanja na walijitahidi kwa uwezo wao mpaka kuwadhibiti vilivyo.

Tafrani hiyo imekuja ikiwa Simba leo wanaingia dimbani kucheza na Nkana ukiwa ni mchezo wa raundi ya pili ikiwa ni baada ya kupoteza ule wa mwanzo kwa mabao 2-1 nchini Zambia.

4 COMMENTS:

  1. Wa Yanga Ni Wapumbavu Kabisa Wana Undugu Gan Na Nkana Ya Zambia Kwa Taarifa Tu Leo Hii Nkana Watapoteza Tena Kwa Goal Nyingi

    ReplyDelete
  2. Ck alie shindwa hutatamani mafanikio ya mwenzake koo YANGA fanyeni vizuri mwakani muweze kucheza c kutuletea ujinga wenu

    ReplyDelete
  3. yaani yanga wameshindwa kufanya kikao jangwani wanataka kufanyia taifa wale kweli vyura

    ReplyDelete
  4. Watanzania wachache wetu wanaupumbavu kama wa bata

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic