MMOJA SIMBA NJE LEO WAKATI IKIMENYANA NA NKANA RED DEVILS, LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Uongozi wa klabu ya Simba umesema utamkosa mchezaji wake mmoja kuelekea mechi ya leo dhidi ya Nkana Red Devils kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kupitia Kocha wa Makipa, Mwarami Mohammed, amemtaja Mohammed Ibrahim 'Mo' kuwa nje ya kikosi kutokana na kuwa majeruhi.
Mo atazidi kukosekana ikiwa ni takribani miezi kadhaa hajacheza ndani ya kikosi akiwa bado hajawa fiti kiafya jambo ambalo linapelekea aendelee kusugua benchi.
Aidha, Mwarami ameeleza maandalizi yote kwa ujumla yamekamilika na wapo tayari kupigana kufa na kupona ili kupata matokeo mazuri leo.
Kocha huyo ametamba kuwa watapigana kwa nguvu zote ili kuweka historia katika michuano hiyo mikubwa kuliko yote kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.
Hakuna Shida Simba Kuna Kikosi Kipana
ReplyDeleteHapana shaka kabisa ushindi wa 3 - 1 upo kwa mnyama, kikubwa wachezaji waipambanie timu mwanzo mwisho. Jamaa hawachomoki. Kule kwao wanalijua hilo ndio maana baada ya mechi ya kwanza walionekana kupoteza matumaini.
ReplyDeletenilikuwa najiuliza mbona Mo Ibrahim hachezi kumbe majeruhi ni pengo kubwa kwani ni mmoja ya wachezaji wanaoweza kubadilisha matokeo
ReplyDelete