December 1, 2018


Kikao cha Kamati tendaji ya klabu ya Yanga kilichokaa leo asubuhi kimewateua Samuel Lukumay kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Klabu hiyo huku Siza Lyimo akiteuliwa kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti.

Uteuzi huo umefanyika kwa ajili ya kusuburia uchaguzi wa kujaza nafasi utakaofanyika January 13 2019.

Kamati hiyo imefikia maamuzi hayo kutokana na nafasi hizo kuwa wazi jambo ambalo liliwa ugumu kwa baadhi ya shughuli ndani ya klabu kwenda sawa.

Wakati huohuo ukiachana na uteuzi, kikosi cha Yanga kimeondoka leo Dar es Salaam kuelekea Mbeya kwa ajili ya mechi ya ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga itapepetuana na Prisons Jumatatu ya wiki ijayo katika Uwanja mkongwe wa Sokoine jijini Mbeya.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic