December 4, 2018



Kikosi cha Mtibwa Sugar, kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Northern Dynamo katika mchezo wa marudio wa kombe la shirikisho Afrika uliochezwa katika visiwa vya Shelisheli.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Chamazi, Mtibwa walifanikiwa kushinda kwa mabao 4-0 hivyo mzigo waliokuwa nao Dynamo leo ulikuwa mzito kuweza kufunga mabao 5-0.

Kwa matokeo hayo Mtibwa wanafanikiwa kusonga mbele katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kufanikiwa kushinda mchezo wa leo ugenini.

Bao la Mtibwa lilifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 68 bada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic