December 4, 2018



Shabiki maarufu wa Simba nchini, Said Khamis maarufu kama Mzee Muchacho amesema anajihisi kama amechanganyikiwa.

Mzee Muchacho anasema anajiona kama amechanganyikiwa kwa furaha aliyoipata baada ya Simba kuitwanga Mbabane Swallows kwa idadi ya mabao 8-1.

Simba imeshinda kwa mabao 4-0 ikiwa ugenini eSwatini ikiwa ni baada ya ule ushindi wa mabao 4-1 jijini Dar es Salaam.

"Nasikia kuchanganyikiwa, hii furaha ya leo haina mfano. This is Simba, waambie hii ndio Simba ya kimataifa.

"Simba inajua nini maana ya michuano ya kimataifa, yaani leo ni furaha ile mbayaa," alisema akionekana ni mwenye furaha sana.

Mzee Muchacho ni kati ya waanzilishi wa kikundi maarufu cha ushangiliaji cha Simba cha Kidede na yeye ndiye amekuwa mpiga tarumbeta lenye sauti maarufu katika soka ya "Po, po, po, popoooo Eeehhh Kidedea".


2 COMMENTS:

  1. Safi sana ni matokeo mazuri ya kutia moyo hongera sana Simba,hongera sana mtibwa sugar.Kama watanzania tumeamua kuwa wazalendo wa kweli basi lazima tuelekeze nguvu zetu kwa mtibwa pia. Katika Dirisha hili dogo la usajili lazima mtibwa iwezeshwe na wachezaji wenye uwezo zaidi wa kupambana kimataifa kwani kazi ndio imeanza katika Tanzania mpya ya ushindani. Kwa upande wa Simba wanaonekana kujiandaa zamani na wapo tayari wanachohitaji ni sapota kutoka kwa watanzania hasa katika kupata taarifa za timu pinzani mapema. Mfano wapinzani wa Simba wanaofuata wanatarajiwa kucheza kesho ni vizuri Simba wakapeleka watu wao kushuhudia mechi hiyo na kama vile kurahisishiwa kazi Simba na baadhi ya viongozi wake bado wapo katika eneo hilo la kusini mwa Africa ambapo wapinzani wao wanaokuja wanacheza kesho. Nnaimani viongozi wa Simba watafanya jitihada za kupeleka watu sahihi wa kushuhudia mechi hiyo ya wapinzani wao wa raundi ya kama si tayari watu hao wa simba wapo huko tayari kutakakochezwa mechi hiyo ili kupata taarifa muhimu. Kila la kheri Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Hakika Simba hii inatia raha, jana usiku hata chakula sijala, kwa sababu ya kushiba ushindi tu, yaani ni furaha tu. Wasioipenda Simba wanastahili kuipenda tu jamani!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic