December 23, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuondolewa jana katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KCCA ya Uganda, uongozi wa Mtibwa Sugar umewataka watanzania kwa ujumla kuipa ushirikiano wa hamasa klabu ya Simba ili ipate matokeo leo dhidi ya Nkana Red Devils.

Simba inashuka dimbani kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili baada ya ule wa kwanza kufungwa mabao 2-1 nchini Zambia.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru, amesema ni wakati mwafaka sasa kuwaunga mkono Simba ikiwa kama timu pekee iliyobaki kwenye mashindano ya kimataifa.

Ameeleza hakuna sababu ya kuanza kuitenga kwakuwa ni sehemu ya taifa na itakuwa inaitangaza Tanzania kisoka na ni vyema wakaiunga mkono ipate nguvu ya kufanya vizuri.

"Watanzania kwa sasa tunapaswa kuipa sapoti Simba ili ifanye vizuri zaidi, niliwaona baadhi ya viongozi jana walikuja Chamanzi kutushangilia lakini bahati mbaya tulitolewa.

"Simba ndiyo timu pekee iliyosalia kwenye mashindano, hatuna sababu ya kuitenga bali vema tukaipa hamasa kubwa iweze kusonga mbele na kufika mbali zaidi, nikipata nafasi nami leo nitaenda Uwanja wa Taifa kuangalia mchezo" alisema Kifaru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic