Moto wa kombe la Shirikisho umeendelea kushika kasi katika viwanja mbalimbali huku timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zikieendelea kupukutishwa kwenye michuano hiyo mapaka sasa timu 5 zimetolewa kwenye mashindano hayo.
Zilizoondolewa mapema ni Mwadui FC ilitolewa na Pan Africa kwa mabao 3-1, Ndanda SC ilitolewa na Tras Camp kwa penati 3-2 baada ya kutoka suluhu dakika 90, Mbao FC ilitolewa na Dar City kwa penati 4-2 baada ya kufungana 1-1.
Tanzania Prisons walitolewa na KMC kwa penati 4-3 baada ya dakika 90 kutoka sare ya kutofungana na Ruvu Shooting walitolewa na Mighty Elephat kwa penati 5-6 baada ya kutoka sare ya kufungana 1-1.
Timu zilizofuzu ni Dar City, Lipuli FC, Singida United, Trans Camp, Pan African, Kagera Sugar, Friends Rangers, Rhino Rangers, Namungo FC, Reha FC, Majimaji FC, Boma FC, Cosmopolitan, Polisi Tanzania, KMC, La Familia, Coastal Union, Mighty Elephant na Alliance FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment