December 22, 2018


Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa kesho anatarajiwa kuanza kazi rasmi ya kuitumikia timu yake mpya baada ya taratibu za usajili kukamilika.

Chirwa amesajiliwa akiwa ni mchezaji huru kwa kandarasi ya mwaka mmoja akitokea timu ya Nogoom ya Misri baada ya kuvunja mkataba kwa kile alichodai kutolipwa stahiki zake.

Ofisa habari wa Azam, Jaffary Maganga amesema, Chirwa anatarajiwa kuanza kuonekana kesho katika mchezo wa Shirikisho dhidi ya Madini utakaochezwa uwanja wa Chamazi.

"Taratibu zote za usajili kwa Chirwa zimekamilika hivyo ni wakati tu na maamuzi ya mwalimu kuweza kumtumia katika mchezo wetu wa kesho dhidi ya Madini ambao ni wa Shirikisho na ule wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.

"Leo ilibidi tucheze na Madini ila kutokana na uwanja kutumiwa na Caf kwenye mashindano ya kimataifa umefanya tuheshimu ratiba na mchezo wetu utakuwa kesho, mashabiki watupe sapoti," alisema.

Mashindano ya kombe la Shirikisho ni mtoano hivyo timu itakayofungwa itatupwa nje ya mashindano hayo ambayo bingwa wake huiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic