December 26, 2018


Baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba walio na uchungu na timu, wameibuka na kuagiza kikosi kilichocheza dhidi ya Nkana kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutumika kwenye kipute cha Kombe la FA leo.

Simba inashuka dimbani kwa mara ya kwanza kucheza mechi dhidi ya Mahsujaa United kutoka mkoani Kigoma ambao pia watakuwa wanaska kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Wanachama na mashabiki hao baadhi wameutaka uongozi na benchi la utani kutofanya utani hata kidogo juu ya mashindano ya FA ili yasije yakawatokea yale ya mwaka jana kwa kufungwa na Green Warriors.

Wengi wameeleza kuwa dharau ndiyo iliwafanya watolewe mapema hivyo hawana budi ya kuhakikisha wanatumia kikosi kipana ili kushinda mechi hiyo.

Aidha, wanachama hao hawakusita kumtaja Rais Magufuli kuwa aliagiza Simba iwe inafanya vema hivyo hawataki kuona kikosi dhaifu kikipangwa kwakuwa Simba itakuwa inacheza na timu ndogo.


2 COMMENTS:

  1. Mwandishi Kakosea Kidogo (Benchi La Utani) Yeah Naungana Na Hao Wanachama Unajua Hata Mm Nawangaa Simba Ukiangalia Kiundani Ni Bora Wangekuwa Wanakataa Kushiriki Kuliko Kujidharaulisha Na Tu Team Tudogo Mf. Mashindano Ya Sportpesa, Kagame Hata Mapinduzi Wamekuwa Wakifanya Utani Mwisho Wake Aibu Et Tuna Kikosi Kipana Sivema Wabadilike Leo Wasiweke Kikosi Cha Ajabu Ajabu

    ReplyDelete
  2. tuna kikosi kipana wachezeshe wale wanaokaa benchi kwa sababu si kwamba wana uwezo mdogo bali upana wa kikosi ndio unawaweka benchi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic