December 21, 2018


Na George Mganga

Aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, ameibuka na kutamba kuwa klabu hiyo bado ni ya kimataifa halisi huku Simba akiwaita ni wa matopeni.

Muro ameibuka baada ya kuwa kimya kutokana na majukumu ya Ukuu wa Wilaya ya Arumeru ambayo alipewa hivi karibuni kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Muro ameeleza hayo ikiwa ni baada ya ushindi wa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon wa bao 1-0 uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

"Unajua sisi bado ni wa kimataifa halisi, mpaka sasa bado hatujapoteza mchezo hata mmoja, tunaendelea kuonesha ukimataifa tofauti na wale wenzetu wa matopeni, ikumbukwe hadi leo hatujapoteza hata mchezo mmoja" alisema Muro.

Aidha, Muro amemtumia salaam Manara alimweleza wajiandae kupokea kipigo kwenye mzunguko wa raundi ya pili akiamini moto walionao Yanga hivi sasa si wa kuotea karibu.

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS 
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa. 
Asante 

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS

5 COMMENTS:

  1. Jipe matumaini tu! Unajisifu kwa kuifunga bao 1 kwa tabu sana timu inayoshika nafasi ya 18!.b Halafu unajitamba kuifunga Simba mzunguko wa pili!

    ReplyDelete
  2. Ulitaka wafungwe bao ngapi
    Au ulitaka Yanga ifungwe
    Usibadili nyeupe kuwa njano

    ReplyDelete
  3. Hivi mzunguko wa pili umeshaanza eeeee?
    Hamjamaliza viporo huku unatamani mechi ya watani ya mzunguko wa pili.

    ReplyDelete
  4. Muro shukuru Mungu kabla ya kuitakia mabaya Simba na kuwaita wa matopeni lakini ujue kuwa haki za wachezaji na marupurupu yanatolewa kila kukicha nanyi mshukuru kuwa mna wachezaji waliostahamili kutekeleza wajibu bila ya kulipwa mishahara lakini itafika wakati watachoka kustahamili njaa na kukimbia na msimamo wa Zahera ndio hapo mmeshaanza kuusikia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic