MWAKYEMBE ATUMA SALAAM KWA WAHUJUMU SERENGETI BOYS, HATAKI UTANI
Na George Mganga
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harisson Mwakyembe, ametoa onyo kwa vilabu vikubwa nchini juu ya kuwanyemelea wachezaji wa Serengeti Boys ili ziwasajili.
Mwakyembe amesema hayo katika hafla fupi iliyoandaliwa na mlezi wa timu hiyo, Reginald Mengi kuwapongeza vijana hao baada ya kutwaa ubingwa wa COSAFA chini ya miaka 17 huko Gaborone, Botswana.
Waziri Mwakyembe amesema baadhi ya timu kubwa zimekuwa na utamaduni wa kuwanyemelea wachezaji hao na baadaye kuwaacha kuwatumia na mwisho wa siku kupoteza ndoto zao.
"Tutakuwa tunawavichukulia hatua timu ambazo zimekuwa na mtindo wa kuwavizia wachezaji hawa wadogo wenye malengo ya kufika mbali hapo baadaye, najua vipo ambavyo tayari vishaanza mazungumzo nao, hatuna utani katika hili" alisema.
Aidha, Mwakyembe pia amewaasa wachezaji hao kuachana na masuala ya anasa ikiwemo starehe na ulevi wa pombe kwani havitawasaidia lolote katika mpira.
BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.
Asante
BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
0 COMMENTS:
Post a Comment