December 4, 2018



Mshambuliaji wa timu ya Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi amesema watahakikisha wanamaliza mapema mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupata matokeo mbele ya Mbabane Swallows FC.

Okwi amesema anatambua wapinzani wao wapo nyumbani na wana hasira ya kupata ushindi hilo haliwapi wasiwasi wamejipanga kiasi cha kutosha.


"Wachezaji wote tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa marudiano na hesabu kubwa ni kupata matokeo, tuliwaona wapinzani na tunajua tuliwafunga bao 4-1 hivyo tutapambana kuvuka hatua ya awali," alisema.


Mbabane na Simba watacheza leo saa 10:00 jioni nchini Eswatini, ili Simba waweze kuvuka hatua ya awali wanapaswa wasiruhusu kufungwa zaidi ya mabao 2.

1 COMMENTS:

  1. Ninachokiamini Simba wapo vizuri zaidi katika mechi hii ya marudiano kuliko na waswati kuliko katika mechi iliyopita. Kurudi kwa Juuko kwenye kikosi,muda wa kutosha wa mkusanyiko wa wachezaji wake katika mazoezi ya pamoja baada ya majukumu yao kwenye timu zao za taifa hasa mshambuliaji wao tegemeo Emanuel Okwi.Lakini kubwa zaidi kwa kocha mzoefu kama Ausems ni ile nafasi yakupata kumjua mpinzani wake jinsi alivyo na namna ya kukabiliana naye ninainani Patrick Ausems yupo vizuri kwa hilo na Swallows lazima wajiandae kisaikolojia kutokana na kile watakachokipata.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic