December 4, 2018



Kocha Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa amewapa mbinu mpya wachezaji wake leo kuweza kupata matokeo mbele ya wapinzani wao Northen Dynamo katika mchezo wa kombe la Shirikisho.

Mtibwa wana kumbukumbu ya kushinda kwa bao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Chamazi hivyo leo wanapaswa kutoruhusu kufungwa zaidi ya mabao 3 ugenini ili kusonga mbele.


"Kwetu sisi ni mwendelezo wa kipindi cha pili licha ya kwamba tutacheza dakika 90 kwa sababu nyumbani tulicheza tukasinda na leo ni marudiano hivyo nimewapa mbinu wachezaji waweze kushinda," alisema.


Jaffary Kibaya alikuwa ni mchezaji wa kwanza kuweka rekodi kwenye mashindano hayo kwa kuwa alifunga 'Hat-trick' waliposhinda bao 4-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic