December 12, 2018




Mshambuliaji wa Simba, Rashid Mohamed, ambaye kwa sasa ametua kwa mkopo KMC, amesema kuwa anatambua ushindani uliopo kwenye ligi na atatumia nafasi hiyo kuonyesha makali yake.

Juzi wakati KMC inalazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Azam FC, Rashind alikuwa jukwaani akisoma mchezo unavyokwenda na kusema kuwa ana uhakika wa kupambana na kusaidia timu hiyo.

 Rashid amesema kuwa kuna changamoto mpya zinakuja kila siku hasa wakati wa kutafuta ila hazimfanyi akate tamaa hasa kutokana na kipaji alichonacho.

"Muda sahihi wa kuweza kukuza na kuonyesha kipaji changu ni sasa, nina imani ya kufanya vizuri hapa nilipo na mashabiki watafurahi wenyewe.

"Kikubwa ni kuwa na nia na kujituma, hakuna namna nyingine miongoni mwa vitu ambavyo havijifichi ni mpira, hivyo nitafanya juhudi kwa kushirikiana na wenzangu ili kuwa bora zaidi," alisema Rashid.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic