December 4, 2018


Baada ya kupoteza pointi tatu nyumbani mbele ya Yanga, kocha msaidizi wa timu ya Prisons, Ismail Seleman amesema kuwa makosa ya mabeki yameigharimu timu.

Prisons wana pointi 10 wamepoteza michezo 7 kati ya 15 waliyocheza wakiwa na sare 6 na wameshinda mchezo 1 pekee.


"Tulianza vizuri na hakukuwa na tatizo kubwa ambalo limetugharimu zaidi ya mabeki kukosa utulivu wakati wa mchezo hali iliyosababisha tuweze kufungwa bao 3-1.


"Tatizo la washambuliaji tumeliona nalo tutalitendea kazi kwa kuwa taratibu wanaanza kuelewa kile ambacho wanatakiwa kufanya hivyo baada ya muda watarejea kwenye ubora," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic