December 31, 2018



REKODI ya kikosi cha Tanzania Prisons msimu huu inawaumiza mashabiki na viongozi kutokana na kushindwa kufurukuta kwa michezo ambayo wamecheza Ligi Kuu.

Prisons walimaliza msimu uliopita wakiwa nafasi ya nne huku Kocha wao Mkuu, Mohamed Abdallah akipewa tuzo ya Kocha Bora wa msimu uliopita.

Kwa sasa Prisons wamecheza michezo 18 wameshinda mchezo mmoja pekee na kutoa sare michezo 9, wamepoteza michezo 8 na kujikusanyia pointi 12 wakiwa nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi hali iliyofanya wamtimue kazi kocha wao.

 Beki wa kikosi hicho Salum Kimenya amesema kuwa wanatambua kazi kubwa waliyonayo katika kupata matokeo hivyo wataongeza juhudi kuweza kujinasua katika nafasi waliyopo kwa sasa.

"Hatupo sehemu nzuri, tuna kazi kubwa kutoka hapa tulipo na njia ni moja tu kupata matokeo mazuri katika michezo yetu mashabiki watupe sapoti," alisema.

1 COMMENTS:

  1. Matatizo ya timu za mikoani ni kutojitambua na kukumbuka shuka asubuhi ...wao wanachojua ni kuzikamia Simba na Yanga ili mchezaji aje asajiliwe na hizo timu.lkn mwisho wa siku wanajikuta wanapigania kutoshuka daraja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic