Mchezo wa Singida United na Coastal Union ya Tanga unatarajiwa kuchezwa Januari 2 katika uwanja wa Namfua, Singinda.
Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema wametambua makosa yao na wamepokea matokeo kinachofuata ni maumivu kwa wapinzani wao Coastal Union.
"Tumepoteza mchezo wetu hilo tunaachana nalo na kuwekeza nguvu zetu kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Coastal Union ambao tutakuwa nyumbani, ni muda wetu kutumia vizuri Uwanja wa nyumbani kupata matokeo chanya," alisema.
Singida United wana pointi 19 wakiwa wamecheza michezo 17 wanashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.








0 COMMENTS:
Post a Comment