December 5, 2018



Baada ya kikosi cha Simba kufanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatimaye watakutana na Nkana FC ya Zambia hivyo watakuwa wanamrudisha nyumbani Chama ambaye anaitumikia pia timu ya Taifa ya Chipolopolo.

Nkana FC ya Zambia anachezea Mtanzania Hassan Kessy ambaye aliwahi kuitumikia timu ya Simba zinatarajiwa kumenyana kwanza Zambia kati ya Desemba 14 na 16 na marudio kuchezwa uwanja wa Taifa kati ya Desemba 21 au 23.


Nkana wamefanikiwa kupenya hatua ya kwanza baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 na kushinda mchezo wa marudiano kwa bao 1-0  dhidi ya  UD Songo ya Msumbiji na kufanya wawe na jumla ya mabao 3-1.


Simba wana jumla ya mabao 8-1 kwa kuwa walishinda mchezo wa kwanza nyumbani kwa mabao 4-1 na ule wa marudio uliochezwa nchini Eswatini alishinda kwa mabao 4-0.

4 COMMENTS:

  1. Mi naitaka tp mazembe maana hao nkana hawana jipya!this is simbaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. ulimshindwa mbao!!!!.....eti leo unamtaka TP Mazembe.....unachekesha sana.....hata kama kiwango chako ni kizuri kwa sasa lakini usijiweke kwenye levo ya TP Mazembe mjomba.

      Delete
  2. Ni maombi tu na juhudi za mazoezi kwa wachezaji pamoja na mbinu kwa benchi la ufundi. Ingawa naiamini Simba hii, hayo pia yatatufanya tuzidi kuimarika zaidi na kuwa na uhakika wa kusonga mbele.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic