December 5, 2018



Kikosi cha Timu ya Yanga leo kimepoteza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki mbele ya timu ya Sumbawanga United mchezo uliochezwa Sumbawanga katika uwanja wa Mandela.

Yanga wamefanikiwa kucheza michezo minne ya kirafiki ambapo walitoa sare tatu na kushinda mchezo mmoja leo wamepoteza mchezo wao wa kwanza kwa kukubali kufungwa mabao 2-1.


Sumbawanga United walikuwa wa kwanza kumrudisha kwenye nyavu Klaus Kindoki dakika ya 6 na Romano Nchimbi na bao la pili likafungwa na John Sabas dakika ya 61 bao la kusawazisha la Yanga lilifungwa na Thabani Kamusoko dakika ya 45.


Michezo ambayo Yanga walicheza ya kirafiki ni pamoja na ule dhidi ya African Lyon walishinda bao 1-0, Reha FC sare ya bao 1-1, Namungo FC sare ya bao 1-1 na Sumbawanga United wamepoteza kwa kufugwa bao 2-1 ikiwa ni baada ya Ligi kuanza.

3 COMMENTS:

  1. Assume ingekuwa ni Simba, title ingeweza kuwa "MNYAMA ATAFUNWA NA TIMU AMBAYO HAIPO KATIKA DARAJA LOLOTE", au MNYAMA ANG'ATWA, au MNYAMA AANGUSHWA NA SISIMIZI" pamoja na titlle zingine kibao za kejeli. Lakini kwa vile ni Yanga titlle imekuwa ya kiulaiiiiiini....

    ReplyDelete
    Replies
    1. si bure......inaonekana dhahiri kuwa wewe ni shabiki"MAANDAZI"

      Delete
    2. Huna tofauti na mwandishi nawe! ndo wale wale wanazi bandia.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic