December 16, 2018


Na George Mganga

Kuelekea mechi ya leo kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting, Kocha Mwinyi Zahera amewataja wachezaji baadhi wa kikosi cha Yanga ambao wataukosa mchezo huo.

Zahera amewataja Thaban Kamusoko, Mrisho Ngassa kuwa sehemu ya wachezaji ambao hawatakuwepo katika kipute hicho.

"Tumejiandaa vyema kuwakabili maana Ruvu Shooting sio timu ndogo na ina uzoefu wakutosha kwenye ligi kuu,wachezaji wangu wote walio kambini wapo sawa kuelekea mchezo wetu wa kesho"

"Kuna baadhi ya wachezaji watakosa mchezo wa kesho kwa matatizo mbali mbali Kamusoko na Raphael Daudi wote hawa ni majeruhi na Mrisho Ngasa yeye bado anatumikia adhabu yake ya kadi Nyekundu pia Yondani ana kadi tatu za njano."

"Ajibu baada ya kukosa mchezo uliopita atakuwa sehemu ya mchezo wa kesho pamoja na mchezaji mmoja Gustavo toka kwenye kikosi chetu cha U20 pia atakuwa sehemu ya mchezo wa kesho."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic