December 25, 2018


Inawezekana yakawa yametimia!!  Taarifa kutoka Uganda zinasema straika wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi amefikia makubaliano binafsi na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Okwi ambaye amecheza soka lake kwa mafanikio ndani ya Msimbazi, ameanza kuhusishwa kutua Kusini mwa Afrika kwa miamba hao wa soka baada ya kuvutiwa na juhudi zake.

Kwa mujibu wa mtandao wa Kawowo Sports kutoka Uganda, umeeleza kuwa Okwi amekubaliana na Kaizer Chiefs huku mazungumzo na mabosi wa Okwi nayo yakiiva.

Kawowo umeeleza kuwa Mabosi wa Okwi ambao ni Simba tayari wameshamalizana na Kaizer ambayo inamhitaji kwa udi na uvumba Okwi hivyo kuna uwezekano akaondoka muda wowote ule Msimbazi.

Licha ya Kazier kumuhitaji Okwi, Kocha Mkuu Patrick Aussems ameweka ngumu kwa mchezaji kutoka kwani hivi sasa anamtegemea kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kama sehemu ya mchango.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic