December 14, 2018


Straika Heritier Makambo wa Yanga hivi karibuni alivunja rekodi yake aliyoiweka ya kufunga mabao saba katika kipindi cha kwanza kwenye kila mechi za timu hiyo baada ya kufunga bao kipindi cha pili na kuifanya Yanga iibuke na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United.

Makambo ambaye sasa ana mabao nane aliandika rekodi ya kufunga mabao saba katika kipindi cha kwanza tena huku akiwa ndiye mtu wa kwanza kufanya hivyo.

Hii ni rekodi ya mchezaji huyo ambayo imewashinda mastaa kadhaa akiwemo Emmanuel Okwi wa Simba ambaye amecheza ligi hii kwa zaidi ya miaka sita.

Kwenye mchezo huo dhidi ya Biashara United uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, Makambo alifunga bao lake katika dakika ya 80 likiwa ndiyo la kwanza anafunga kipindi cha pili tangu ametua nchini.

Pia katika mchezo huo Makambo alishindwa kuendeleza rekodi yake ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao la kwanza baada ya beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kuwa ndiye mchezaji wa kwanza kupachika bao la kwanza.

Makambo alifunga mabao yake kipindi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Coastal Union, Lipuli FC, JKT Tanzania, Alliance Schools, Kagera Sugar, Mwadui FC.

5 COMMENTS:

  1. tumia akili tangu mara ya mwisho Okwi acheze ligi kuu bara si ameishafunga magoli? Je ni mechi ngapi za ligi bara makambo ameishacheja.Ngoja nikukumbushe wewe usiyefikiria au unayesahau.. Makambo ana mechi tatu zaidi ya Okwi.. Mara nyingi kufikiria sio kazi sana.. na uhitaji akili nyingi..kwa hili hata kondoo atafanya kazi nzuri zaidi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnaandika pumba...mkiambiwa ukweli mnasema povu...hivi na akili zako alichoandika mwandishi kina fikira kweli...mwandishi anavyosasambua ni sawa na darasa la pili!hajui kabisa kufikiria

      Delete
  2. Stori hii mmelazimisha tu. Huwezi kumlinganisha Okwi na huyo mwanamuziki wa Yanga.

    ReplyDelete
  3. bila kuamdika simba mnajua kabisa watu hawasomi habari zenu Makambo kitu gani kwa Okwi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic