December 18, 2018


Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsaini kiungo mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uhispania Isco, 26, baada ya msimu kukamilika. Tayari mazungumzo ya awali kati ya miamba hao wa England na mchezaji huyo yameshafanyika. (As - in Spanish)

Manchester United itawapasa kutoa kitita cha pauni milioni 24 kama wataamua kumfuta kazi kocha wao Jose Mourinho kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. (Daily Record)

Kiungo wa zamani wa Liverpool Danny Murphy amesema muda wa kumfuta kazi Mourinho ni huu. (Talksport)

Wakuu wa ligi ya Premia wanataka kufanya mazungumzo na wachezaji weusi ili kutafuta njia bora za kupambana na ubaguzi mchezoni - wachezaji weusi wanatazamiwa kuvigomea vyombo vya habari kama sehemu ya mapambano dhidi ya ubaguzi. (Mirror)

Klabu ya Chelsea inajipanga kuwafungia mashabiki wanaofanya ghasia nje ya uwanja wao wa Stamford Bridge kutohudhuria mechi za klabu hiyo. Hivi majuzi, klabu hiyo imewafungia kwa muda kupisha uchunguzi mashabiki wake wanaodaiwa kumtolea shutuma za kibaguzi nyota wa Manchester City, Raheem Sterling. (The Times)

Klabu ya Juventus imekutana na wakala Mino Raiola kuzungumzia uhamisho wa mchezaji nyota Paul Pogba wa Manchester United. Pia mazungumzo hayo yamehusisha usajili wa mlinzi kinda wa Ajax Matthijs de Ligtmet mwenye miaka 19 na kuongeza mkataba wa mshambuliaji kinda wa Italia mwenye miaka 18 Moise Kean. (Sky Italia via Football Italia)

Paul Pogba, alisajiliwa na Manchester United kwa kima cha pauni Milioni 89 akitokea Juventus. Vigogo hao wa Italia wanataka kumrejesha Pogba jijini Turin baada ya kubaini kuwa United wanataka kumuuza katika dirisha la usajili la mwezi Januari. (Tuttosport via Mirror)

Beki raia wa Ujerumani anayekipiga katika klabu ya Chelsea Antonio Rudiger, 25, amesema bado hajaongea na uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake jijini London kuhusu kuongeza muda wa kandarasi yake. (Metro)

Manchester United ni moja ya vilabu vilivyoonesha nia ya kumsajili beki kinda wa Galatasaray raia wa Uturuki Ozan Kabak mwenye miaka 18. (Daily Mail)

Barcelona wamepokea ofa ya paui milioni 65 kutoka vilabu vya ligi ya Uchina vinavyotaka kumsaini mshambuliaji wao rai wa Brazil Malcom mwenye miaka 21. (As - in Spanish)

Majeraha yaliyompata beki raia wa Ubelgiji anayechezea Barcelona Thomas Vermaelen, 33, yanaifanya klabu hiyo kuwa na kila sababu ya kutafuta beki mpya wa kati. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic