Beki kinda wa timu ya Yanga, Paul Godfrey amesema wapo tayari kuvaana na African Lyon katika mchezo wao wa Ligi Kuu utakaopigwa mkoani Arusha siku ya alhamisi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Yanga wamefanikiwa kufanya vizuri kwenye michezo yao 16 waliyocheza mpaka sasa bila kupoteza hata mchezo mmoja.
"Tupo sawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya African Lyon, hatuna mashaka kwa kuwa tayari tumeshapewa mbinu mpya zitakazosaidia kutupa matokeo.
"Mafanikio yetu yanabebwa na ushirikiano wa timu hivyo mashabiki watupe sapoti katika mchezo wetu kwani tunaamini kufanya kwetu vizuri wao pia wanachangia kwa kiasi kikubwa," alisema.
Yanga wamefikisha pointi 44 na imejikita kileleni kwa kuwaacha wapinzani wao Simba kwa tofauti ya pointi 17 huku Simba wakiwa na viporo vinne.
0 COMMENTS:
Post a Comment