December 3, 2018



Wachezaji wawili leo wamepewa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara unaochezwa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kati ya Tanzania Prisons na Yanga kwa kile ambacho mwamuzi ametafsri kuwa utovu wa nidhamu.

Wachezaji hao ambao ni Mrisho Ngasa wa Yanga na  Laurance Mpalile wa Prisons baada ya kukosa nidhamu katika mchezo huo leo dakika ya 45.


Ngasa alionekana akimpiga kichwa mchezaji mmoja wa Prisons mbele ya mwamuzi na baada ya mwamuzi kupuliza filimbi Mpalile alionekana akimpiga kichwa Ngasa mbele ya mwamuzi.


Mpira unaendelea ikiwa ni kipindi cha pili na timu zote zinacheza zikiwa na wachezaji 10 uwanjani kutokana na wachezaji kupewa kadi nyekundu.


Prisons wanakubali kupoteza mchezo wao katika uwanja wa nyumbani kwa kufungwa bao 3-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic