January 26, 2019


Ligi Kuu Bara sasa imefikia mahali patamu kwa timu zinazowania ubingwa na zile zinazopambana ili zisishuke daraja na zinapigana kwelikweli ili kutimiza ndoto zao.

Misimu ya hivi karibuni tumekuwa tukiona timu ikitwaa ubingwa huku ikiwa na mechi mbili, tatu au zaidi mkononi lakini msimu huu mambo ni tofauti na kabla ya mechi ya jana hakuna timu iliyokuwa na uhakika wa ubingwa.

Katika mechi hizi za mzunguko wa pili ambako ndiko tunaenda kwenye ushindani wa hali ya juu zaidi kwa timu kuwania ubingwa na nyingine kukazana ili zisishuke daraja ni vyema Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakawa macho.

Mwishoni kumekuwa na mambo mengi ya upangaji matokeo na mengine yasiyofaa katika soka letu hutokea hivyo ni lazima wahusika wajipange kuhakikisha vitu hivi havitokei.

Haitakuwa vizuri timu ikatwaa ubingwa kwa njia zisizofaa au timu kushuka daraja kwa kuhujumiwa na klabu nyingine, soka ni mchezo wa kuburudisha siyo wa kujengeana uhasama usiofaa. Tunaamini TFF na Bodi ya Ligi ina watu makini watakaosimamia mechi hizi za mwisho kwa umakini ili kutenda haki kwa kila mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic