January 22, 2019


Wapenzi wengi wa soka wanapozungumzia tukio la Simba kuivua ubingwa na kuitupa nje ya michuano ya klabu bingwa afrika mwaka 2003 mabingwa wa zamani wa michuano hiyo timu ya Zamalek ya Misri.

Wachezaji wanaotajwa sana ni marehemu Christopher Alex Massawe kwa sababu yeye ndiyo alipiga penati ya tano na ya mwisho ambayo iliipa uhakika simba kutinga hatua ya makundi na golikipa Kaseja Juma kaseja kwa kuwa yeye aliokoa penati mbili kati ya tatu walizokosa.

Lakini hakuna anayemtaja kijana wa kinyakyusa mrefu, mweusi na mpole Emmanuel Gabriel Mwakyusa ukipenda muite Batgol ambaye alisajiliwa Simba mwaka 2001 akitokea timu ya Nazareth ya Njombe.

Yeye ndiye aliitanguliza Zamalek ICU baada ya kuifungia Simba bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam hivyo kuitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye mchezo wa marudiano.

Simba ilifungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa marudiano nchini Misri hivyo kupelekea matokeo ya jumla kuwa sare ya bao 1-1 hapo ndipo hatua ya kupigiana penati ilipofuata.

Kama haitoshi mara baada ya Simba kufanikiwa kuingia hatua ya makundi Gabriel ndiye aliyekuwa mshambuliaji tegemeo zaidi kwenye ufungaji akifunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Enyimba kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa uhuru. 

Ikumbukwe kwenye mchezo dhidi ya ismailia hatua hiyo hiyo ya makundi gabriel alifunga bao moja maridadi sana kwa kichwa akiunganisha krosi ya beki Boniface Julius Joseph Pawasa kwa mshangao wa wengi Mwamuzi toka nchini Msumbiji alilikataa bila kufafanua ni off side au la.

Gabriel ambaye alikuwa na uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji kama alivyotumika kwenye mchezo wa fainali ligi ya muungano dhidi ya Mlandege kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar baada ya kiungo halisi chotara Shekhan Rashid kutimkia nchini Sweeden siku chache kabla ya mchezo huo ambao Simba ilishinda bao 1-0 na kutwaa ubingwa huo mwaka 2002.

Mkali huyo wa kucheza mtindo wa dansi maarufu "kiwazenza" kama alivyocheza march 31 '2002 baada ya kuifungia Simba bao la nne dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa fainali kombe la Tusker ameipa Simba mataji 11 pia akiifungia mabao matano kwenye za watani wa jadi.

Aliibuka mfungaji bora wa kombe la Tusker mwaka 2003 akifunga mabao matano

Ligi kuu 2001, 2003 na 2004
Ligi ya muungano 2001 na 2002

Kombe la kagame moja mwaka 2002

Kombe la tusker 2001, 2002, 2003, 2005 na 2005 hili lilifanyika nairobi nchini kenya

HUYO ndiyo Emmenuel Gabriel mmoja wa wachezaji nembo ya Simba Sports Club walioitendea haki jezi namba 10 inayoonekana nzito kwa Adam Salamba.

Na Abubakar Mohammed Mbwana

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic