KOCHA mkuu wa Lipuli FC ya Iringa, Selemani Mtola ameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kulitaka kuwa makini katika mzunguko wa
pili kutokana na baadhi ya mechi kutorushwa ‘live’.
Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara umenza kutimua vumbi hivi
karibuni ambapo baadhi ya timu zimecheza mechi tatu huku nyingine zikicheza
mechi mbili na Simba bado ina viporo vyake vinne vya mzunguuko wa kwanza wa
ligi kuu baada ya kucheza mechi 14 tu hadi sasa.
Matola amesema kuwa, mechi za mzunguuko wa pili zimeanza kuwa na
dosari kutokana na baadhi ya mechi kutoonyeshwa ‘live’ hivyo kuwaruhusu waamuzi
kufanya mambo ndivyo sivyo hivyo kuharibu ligi kwa ujumla.
“Mzunguko wa pili umeanza vizuri na kumekuwa na ushindani wa hali
ya juu, lakini kuna dosari ambayo imeingia ya baadhi ya mechi kutoonyeshwa
‘live’ hivyo TFF inatakiwa kuwa makini katika suala hilo
ili kuifanya ligi iendelee kuwa na mvuto kama awali.
“Wakati mechi zote zilivyokuwa zinaonyeshwa live ilisaidia
kupunguza uonevu kwa kiasi fulani kutokana na wahusika kuhofia kuonekana,
lakini katika kipindi hiki cha pili kuna mechi zimekuwa hazionyeshwi ‘live’ na
kuna waamuzi wameanza kufanya michezo michafu kwa timu kadhaa kulalamika
kufanyiwa ndivyo sivyo.
“Ligi inapokwenda inaelekea pabaya, hali hii ilipotea sasa
inajirudia, TFF inatakiwa kuwa makini sana katika mzunguuko wa pili ili ligi
iwe na mvuto na kusiwe na uonevu,” alisema Matola.
0 COMMENTS:
Post a Comment