January 26, 2019


SIMBA wanatambua kwamba kwa sasa nahodha wa Yanga, Ibrahim Ajibu ndiye kinara wa pasi za mwisho Ligi Kuu Bara  ambapo mpaka sasa anazo 14 hali iliyowashtua viongozi Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema katika wachezaji wa Yanga ambao anakubali uwezo wao ni pamoja na Ajibu ila anashangazwa na uwepo wake ndani ya Ligi Kuu Bara.

"Ajibu ni mchezaji mzuri na anatambua kazi yake akiwa Uwanjani hali ambayo inafanya nami nikubali kazi yake hata viongozi wa Simba wanatambua kwamba ninamkubali kwa hapa bongo.

"Bado nashangwaza na uwepo wake hapa bongo kwa kuwa kutokana na udambwiudambwi ambao anaonyesha akiwa Uwanja wa Taifa ana nafasi ya kuwa nje kuonyesha uwezo wake nashangaa kumuona bado yupo bongo," alisema Manara.

Manara ana mpango wa kuzindua kampuni yake ya Manara Foundation ambayo ina lengo la kuwasaidia watu wa makundi maalumu ataifanya kesho katika hotel ya Hyatt Regency amewaalika watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Yanga kama Dismas Ten na Ajibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic