January 26, 2019

BAADA ya Yanga kutolewa mapema kwenye hatua ya robo fainali ya SportPesa Cup, uongozi umesema nguvu zote za timu kwa sasa ni kwenye mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kikosi chao kwa sasa kimeanza kujipanga kwa ajili ya mchezo wao muhimu huku hesabu zikiwa kupata matokeo chanya yatakayowafanya wasonge mbele kwenye michuano hiyo.

"Ni mchezo muhimu kwetu, tunaamini tukipata matokeo chanya tutasonga mbele, wachezaji wana morali tayari wameshaanza maandalizi kwa ajili ya mchezo huo, walianza kufanya hivyo mara baada ya kuondolewa kwenye michuano ya SportPesa Cup na KK Sharks.

"Mchezo wetu utachezwa January 31 Uwanja wa Taifa hivyo mashabiki wanapaswa waelewe na siyo vinginevyo kama ambavyo wamekuwa wakisikia, tutakuwa nyumbani kwenye Uwanja wetu wa nyumbani sapoti muhimu," alisema Ten.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic