January 22, 2019


Simba kwa sasa inafanya mchakato wa kuhakikisha inamsajili pacha wa mshambuliaji tegemeo kikosini humo, Meddie Kagere, Jacques Tuyisenge. Tusiyenge na Kagere ndio waliokuwa wakiunda safu ya ushambuliaji ya Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton uliochezwa hapa nchini mwaka juzi.

Everton ilishinda mabao 2-1, mabao yao yakifungwa na Wayne Rooney pamoja na Kieran Dowell huku Tuyisenge akifunga bao pekee la Gor Mahia. Katika kuhakikisha kikosi cha timu hiyo kinakuwa vizuri zaidi uongozi wa Simba uko kwenye mipango ya kimyakimya ya kumuongeza nyota imara kikosini hapo na sasa inakomaa na Jacques Tuyisenge.


Simba chini ya mwekezaji wake, Mohammed Dewji ‘Mo’ inaelezwa imefikia hatua nzuri na mchezaji huyo wa Gor Mahia na kuna uwezekano mkubwa akatua Msimbazi kabla ya msimu wa Ligi Kuu Bara kumalizika. “Viongozi wanaendelea kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji ili utakapofika muda wa usajili wasije kumbana na wakati mgumu.

“Mmoja wa wachezaji ambaye uongozi unaendelea kufanya mazungumzo naye ni Tuyisenge ambaye mkataba wake na Gor Mahia utamalizika hivi karibuni ,kupitia kwa wakala wake ambaye pia ndiye wakala wa Kagere, ili kuhakikisha naye anatua Simba kuungana na ndugu yake,” kilisema chanzo chetu cha kuaminika.

Kutokana na hali hiyo, Championi Jumamosi lilimtafuta wakala wa Tuyisenge, Patrick Gakumba ambaye alisema: “Mpango huo upo lakini kwa sasa sipo tayari kusema chochote.”

CHANZO: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Yaani kwakuwa tu mmeona.wachezaji waliofika nakufanya mazoezi matimu mdio baas kwenu kumekucha na mmeshaanza tetesi zausajili,mbona hamkuzungumzia hao waliotua mpaka wapo mazoezini ndio mnaibuka nawengine

    ReplyDelete
  2. Mipango ya ajabu kana kwamba timu haina viongozi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic