LEO michuano ya SportPesa Cup inatarajiwa kuanza Uwanja wa Taifa ikiwa ni hatua ya robo fainali ambapo timu nne zitashuka kumenyana ili kuttafuta timu itakayofika hatua ya nusu fainali.
Timu ya Singida United itarusha karata yake ya kwanza saa 800 mchana dhidi ya Bandari na Yanga itacheza na KK Sharks majira ya saa 10:00 jioni.
Bingwa atapewa zawadi ya dola 30,000 na kupata nafasi ya kucheza na timu ya Everton nyumbani kwa mshindi na mshndi wa pili atajinyakulia dola 10,000 na mshindi wa tatu atajinyakulia dola 5,000.
Kiingilio katika michezo yote miwili ya leo bei ya kawaida ni 2,000, VIP B na C 5,000 na VIP A ni 10,000
0 COMMENTS:
Post a Comment