January 15, 2019


NAHODHA wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu anaanza na rekodi yake leo katika mchezo wake wa kwanza akiwa amevaa kitambaa cha unahodha baada ya kufunga bao la kwanza katika mchezo wao wa ligi dhidi ya Mwadui Uwanja wa Taifa.

Ajibu amefanikiwa kuandika bao hilo baada ya kupiga faulo akiwa nje ya 18 dakika ya 12 ikamshinda mlinda mlango na kuzama moja kwa moja langoni.

Dakika ya 18 Yanga walipata penati baada ya Tambwe kuchezewa rafu eneo la hatari ila Penalti hiyo ilipigwa na Ajibu iliokolewa na mlinda mlango wa Mwadui Anold Masawe.

Dakika 39 Ajibu alimpa pasi ya bao Amiss Tambwe akamalizia kwa kichwa na kipindi cha pili dakika ya 57 Fei Toto anafunga bao la tatu akimalizia pasi ya Ajibu.

Dakika ya 82 Mwadu wanapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Salum Aiyee akimalizia pasi ya Ditram Nchimbi.


2 COMMENTS:

  1. Mwambieni Kocha Yanga aifunde defense yake....makosa mengi MNO....YAANI IKIPATA MPINZANI MWENYE FORWARD KALI HABARI ITABADILIKA

    ReplyDelete
  2. Jamani watani kwa kweli mnamwenendo mzuri sana, ninachokiona mm kwa soka la kibongobongo ninaona kama watani mnanafasi ya kutwaa kikombe sasa nawaasa acheni swaga za kusema et ninyi ni ombaomba kumbe ninyi ni matajiri wa kutupwa ila viongozi wenu ndo wanawaangusha na kupiga pesa wakichukua kipengele kwamba yanga ni masikini, Fanyeni usajili kwa ajili ya maandalizi ya kimataifa na mbinu za kuiendeleza klabu, najua kwa juhudi mnazozionesha kiukweli hamuwezi kukoswa vikombe vyote lazima mtaiwakilisha nchi tu. Jipangeni kisawasawa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic