January 15, 2019


KOCHA mpya wa Singida United, Mserbia Dragan Popadic ambaye aliwahi kuifundish Simba, amepewa mtihani mzito wa kufanikisha kupata matokeo mazuri kwa kushirikiana na Dusan Momcilovic ambaye ni Kocha Msaidizi ndani ya kikosi hicho ambacho kimekuwa na mwenendo mbovu kwa msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara.

Singida United inashika imecheza michezo 20 na kufanikiwa  kushinda michezo sita wamepoteza michezo nane na wametoa sare michezo sita na kukusanya pointi 24.

Katibu Mkuu wa Singida United, Festo Sanga amesema wamempa masharti magumu kocha huyo ili aweze kuisaida timu kuleta ushindani kwenye Ligi pamoja na kombe la SpotPesa Cup ambalo linatarajiwa kuanza januari 22.

"Mabadiliko ya kwenye benchi letu lote la ufundi yana malengo chanya kwani tuahitaji kupata matokeo chanya na tumempa taarifa kocha wetu mpya kile ambacho tunahitaji akitimize kwa wakati.

Popadic amesema anatambua ushindani uliopo ndani ya soka la Tanzania ana imani ya kupata matokeo chanya kikubwa na kuomba ushirikiano ili kufikia malengo ambayo wanahitaji ndani ya kikosi hicho.


1 COMMENTS:

  1. Dah kocha Popadic alikuwa mmoja wa makocha bomba sana na kwa hakika alikubalika Msimbazi.Nakumbuka safu ya ulinzi ilikuwa haipitiki kirahisi na mpira ulikuwa unaanzia kwa Mwameja ikiwa na kina Masatu, Masha na wengineo waliotangulia mbele ya haki...kwa kweli walikuwa wanatoa burudani maridhawa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic